Kitengo cha mahusiano kimekamilisha maandalizi ya kongamano la (Miezi ya Muhammadiyya) katika mji wa Waasit

Kitengo cha uhusiano katika Atabatu Abbasiyya, kimekamilisha maandalizi ya kongamano la (Miezi ya Muhammadiyya) katika mkoa wa Waasit.

Kongamano linasimamiwa na idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule chini ya kitengo, kupitia mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, kwa kushirikiana na kitivo cha malezi katika chuo kikuu cha Waasit, kama sehemu ya kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa watakatifu katika mwezi mtukufu wa Shabani.

Kiongozi wa idara ya harakati za vyuo vikuu Sayyid Mustwafa Falaah Arsaan amesema: “Maandalizi yamehusisha kukamilisha mpangilio wote wa kiufundi”, akabainisha kuwa “Ni sehemu ya ratiba za kitamaduni zinazosimamiwa na Ataba tukufu katika vyuo vikuu, kwa lengo la kuimarisha misingi ya kiislamu na kitamaduni kwa wanafunzi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: