Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya semina ya kuwajengea uwezo watumishi wapya.
Mkufunzi wa semina Sayyid Mustwafa Alhakiim amesema, “Semina inamada tofauti za kimaadili kwa watumishi wapya, sambamba na kuwafundisha mbinu za kuamiliana na zuwaru na kubainisha mfumo kamili wa kiutendaji”.
Akaongeza kuwa “Semina imefanywa katika majengo ya Shekhe Kuleini chini ya Atabatu Abbasiyya, itadumu kwa muda wa siku nne, kila siku saa tatu za masomo”, akasema kuwa “Itahitimishwa kwa kuwapa jaribio la kupima unufaikaji wa washiriki”.
Akabainisha kuwa “Semina inalenga kuandaa watumishi wenye uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi chini ya mtazamo wa Atabatu Abbasiyya na misingi bora ya utumishi, kwa ajili ya kutoa huduma bora zaidi kwa zuwaru”.







