Sayyid Swafi azawadia washiriki wa kikao cha ufunguzi wa kongamano la kuadhimisha miaka elfu moja ya hauza ya Najafu-Ashrafu

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amegawa zawadi kwa washiriki wa kikao cha ufunguzi wa kikao cha kwanza katika kongamano la kuadhimisha miaka elfu moja tangu kuanzishwa kwa hauza ya Najafu-Ashrafu.

Kongamano linasimamiwa na kituo cha tafiti na uhakiki cha Shekhe Tusi, chini ya kamati kuu ya kuhuisha turathi za Ataba tukufu, kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Alkafeel na Maahadi ya tafiti za kishia – Toronto, chini ya kauli mbiu isemayo (Hauza ya Najafu-Ashrafu: miaka elfu moja ya utoaji elimu) na anuani isemayo (Turafhi za Shekhe Tusi katika fikra za kiislamu na kimagharibi, ukaribu na usasa) katika jengo la Imamu Mrtadha (a.s) chini ya Atabatu Abbasiyya katika mji wa Najafu.

Miongoni mwa waliopewa zawadi ni rais wa kikao Dokta Shekhe Haidari Sahalani na watafiti, Muheshimiwa Sayyid Muhammad Jawaad Shabiri Zanjaani mwalimu wa Bahathul-Khariji katika hauza ya Qum, mtafiti Dokta Matiyu Tirin, mkuu wa tafiti katika chuo kikuu cha Parisi nchini Ufaransa.

Atabatu Abbasiyya huonyesha mafanikio ya wanachuoni wakubwa katika matukio tofauti ya kielimu, kwa kufanya uhakiki, usambazaji, nadwa, kongamano, kuonyesha machapisho ya turathi, vitabu vya kielimu vinavyo angazia urithi na utukufu wa hauza ya Najafu-Ashrafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: