Atabatu Abbasiyya imewapa zawadi washiriki wa kongamano la kuadhimisha miaka elfu moja ya hauza ya Najafu-Ashrafu

Atabatu Abbasiyya imewapa zawadi watafiti walioshiriki kwenye ratiba ya kongamano la kuadhimisha miaka elfu moja ya hauza ya Najafu-Ashrafu.

Waliosimamia ugawaji wa zawadi kwa niaba ni, mwalimu wa Bahthul-Khaarij katika hauza ya Qum Muheshimiwa Sayyid Muhammad Jawaad Shabiri Zanjani, mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Dokta Abbasi Didah Mussawi na rais wa chuo kikuu cha Alkafeel Dokta Nuris Dahaani.

Kongamano limesimamiwa na kituo cha utafiti na uhakiki cha Shekhe Tusi, chini ya kamati kuu ya kuhuisha turathi za Atabatu Abbasiyya, kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Alkafeel na Maahadi ya tafiti za kishia chini ya kauli mbiu isemayo (Hauza ya Najafu-Ashrafu: miaka elfu moja ya utoaji wa elimu) na anuani isemayo (Turathi za Shekhe Tusi katika fikra za kiislamu na kimagharibi: ukaribu wa sasa).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: