Kitengo cha miradi ya kihandisi kimeanza kujenga kituo cha kusafisha maji karibu na Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f)

Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kimeanza kujenga kituo cha kusafisha maji karibu na Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f).

Mhandisi mkazi katika mradi huo, Sayyid Hussein Muhammad Baaqir amesema “Watumishi wa kitengo wameanza ujenzi wa kituo cha kusafisha maji, nyuma ya Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f), ili kupata maji safi ya kunywa zuwaru wa malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), sambamba na wakazi wa mji huo, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha mji wa zamani unaofanywa na Ataba tukufu, unaolenga kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma”.

Akaongeza kuwa “Kituo kitasaidia upatikanaji wa maji safi ya kunywa baada ya kusafishwa kwa ustadi na umaridadi mkubwa, na kumaliza uhaba wa maji”.

Akasema kuwa “Kituo hicho ni moja ya vituo vinavyosimamiwa na kitengo ndani ya mji wa zamani, kupitia mradi wa uboreshaji wa mazingira unaoendana na mkakati wa Ataba wa kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa zuwaru na kuboresha huduma”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: