Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya kongamano la Ainul-Hayaat katika kitongoji cha Majrul-Kabiir mkoani Misaan.
Kongamano limesimamiwa na kituo cha Multaqal-Qamaru chini ya kitengo, kwa kushirikiana na Hema la uombolezaji wa Bibi Zaharaa (a.s) na kuhudhuriwa na kundi kubwa la viongozi wa kidini, kitamaduni, kijamii na wakazi wa mji huo.
Kongamano limepambwa na usomaji wa Qur’ani, ukafuata ujumbe wa muwakilishi wa Marjaa Dini mkuuu katika mji huo Sayyid Hashim Shara’a, amesisitiza umuhimu wa kufanya makongamano haya na nafasi yake katika kujenga uelewa wa kidini, na kujenga misingi imara katika jamii, kisha ukafuata ujumbe wa kituo uliowasilishwa na Shekhe Mustwafa Idaani, akabainisha malengo ya makongamano na ujumbe wake, pamoja na program mbalimbali za kitamaduni.
Kongamano likahitimishwa kwa kufungua vituo vya kitamaduni, na kuanza kupokea watu wanaokuja kuvitembelea, vituo vimepata muitikio mkubwa na vimekubalika na wahudhuriaji, aidha wameonyesha kufurahishwa kwao na shughuli za kongamano.







