Rais wa kamati ya malezi na elimu ya juu amekagua maendelea ya kielimu katika chuo kikuu cha Al-Ameed

Rais wa kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya na mjumbe wa kamati kuu Dokta Abbasi Didah Mussawi, wamekagua maendeleo ya kielimu katika chuo kikuu cha Al-Ameed.

Wamefanya hivyo walipotembelea chuo na kukutana na rais wa chuo Dokta Judat Nuri Jash’ami, na kukagua ratiba za masomo, sambamba na kutafuta njia za uboreshaji wa mazingira ya kielimu kwa namna ambayo inaendana na malengo ya chuo.

Wakasisitiza ulazima wa kuboresha kiwango cha elimu na kusaidia harakati za kitafiti kwa kuweka mazingira bora kwa walimu na wanafunzi, jambo ambalo linaendana na malengo ya chuo.

Ziara hiyo ni sehemu ya kuboresha utendaji wa kitaasisi na kukuza kiwango cha elimu, pamoja na kuboresha mazingira ya walimu na wanafunzi na kuwawezesha kuhudumia jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: