Kitengo cha Dini kimehitimisha semina ya 57 ya kuwajengea uwezo watumishi wapya wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, kimehitimisha semina ya 57 ya kuwajengea uwezo watumishi wapya wa Atabatu Abbasiyya katika majengo ya Shekhe Kuleini.

Rais wa kitengo Shekhe Swalahu Karbalai amesema: “Kitengo cha Dini kinaendelea na semina za kuwajengea uwezo watumishi wa Ataba tukufu katika masomo ya Fiqhi”.

Akaongeza kuwa “Semina imepambwa na mihadhara ya Fiqhi, Aqida, Akhlaq na mawaidha elekezi, yanayosaidia kujenga heshima ya mtumishi na kumfanya kuwa muwajibikaji bora”.

Akabainisha kuwa, “Semina imedumu kwa muda wa siku sita na imehitimishwa kwa jaribio la nadhariyya, lilikuwa na mada za hukumu za twahara, swala na baadhi ya mambo yanayohitajiwa na mtumishi katika maisha yake”.

Kitengo cha Dini hufanya semina hizi kwa lengo la kujenga uwelewa wa mambo ya kidini kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: