Kitengo cha ufundi kimekamilisha kazi ya kuandaa jukwaa la hafla ya kuwajibikiwa na sharia awamu ya nane

Kitengo cha ufundi chini ya Atabatu Abbasiyya, kimekamilisha kazi ya kuandaa jukwaa la hafla ya kuwajibikiwa na sheria awamu ya nane katika majengo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Hafla ya kufikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria inafanywa kwa kushirikiana na idara ya malezi ya mkoa wa Karbala, kupitia mradi wa maua ya Fatwimiyya awamu ya nane, chini ya kauli mbiu isemayo (Hijabu yangu inatokana na mwenendo wa Zaharaa na kiigizo changu Zainabu) kwa ushiriki wa zaidi ya wanafunzi elfu 6 kutoka shule tofauti hapa mkoani, inafanywa siku ya tarehe 16 – 17 mwezi huu wa pili.

Makamo rais wa kitengo Mhandisi Ammaar Swalahu Mahadi amesema, watumishi wa kitengo wamemaliza kazi ya kutengeneza jukwaa la hafla ya kuwajibikiwa na sheria awamu ya nane katika majengo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) chini ya Ataba tukufu, jukwaa limetengenezwa kwa chuma, mbao, limetandikwa zulia na kuwekwa mfumo kamili wa taa.

Akaongeza kuwa, jukwaa linaukubwa wa mita 29 urefu na upana wa mita 6, akabainisha kuwa kitengo kimeweka mabango ya kukaribisha washiriki na wageni kwenye milango, kimetengeneza jukwaa mbili maalum za wanafunzi, zenye urefu wa mita 10 na upana wa mita 3.

Akafafanua kuwa, maandalizi hayo ni sehemu ya mkakati maalum ulioandaliwa kwa kushirikiana na vitengo tofauti katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: