Mheshimiwa Sayyid Swafi amepiga picha na wanafunzi katika hafla ya kufikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria awamu ya nane

Siku ya kwanza katika hafla ya kufikisha umri wa kuwajibikiwa na sharia katika Atabatu Abbasiyya, imepambwa na ratiba ya upigaji wa picha ya Sayyid Ahmadi Swafi na wanafunzi hao.

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na ofisi ya malezi ya mkoa wa Karbala, kupitia mradi wa maua ya Fatwimiyya, chini ya kauli mbiu isemayo (Hijabu yangu inatokana na mwenendo wa Zaharaa na kiigizo changu Bi Zainabu), kwa ushiriki wa zaidi ya wanafunzi elfu sita kutoka shule tofauti za hapa mkoani.

Ratiba ya siku ya kwanza imepambwa na upigaji wa picha, kusoma kiapo cha kuwajibikiwa na sheria, kuangalia filam ya maua ya Fatwimiyya, igizo na uimbaji wa qaswida za kishairi.

Hafla ya kuwajibikiwa na sheria inayofanywa na Atabatu Abbasiyya, inalenga kuimarisha uelewa wa kidini, utamaduni, misingi ya kiislamu na kutengeneza kizazi kinachojitambua na kuwajibika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: