Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imehitimisha semina ya kuwajengea uwezo walimu wa mradi wa Qur’ani tukufu.
Msimamizi wa semina na kiongozi wa idara Tahfiidh katika Maahadi ya Qur’ani tukufu mjini Karbala chini ya Majmaa, Shekhe Ali Rabii amesema: “Maahadi imehitimisha semina ya kujenga uwezo awamu ya tatu, wameshiriki walimu 55 waliobobea katika somo la kuhifadhi Qur’ani tukufu kutoka matawi ya Majmaa-Ilmi yaliyopo kwenye mikoa tofauti”.
Akaongeza kuwa “Semina ilikuwa na mihadhara tisa kutoka kwa wahadhiri saba, mada zimejikita katika maudhui za elimu ya nafsi, sababu za kuhifadhi, ubao wa hukumu, mbinu za ufundishaji, maarifa ya Qur’ani, mihadhara jumuishi, malezi na hukumu za usomaji”.
Akabainisha kuwa “Semina inalenga kujenga uwezo wa walimu katika kusimamia hilaqa za wanafunzi, na kujenga jamii salama ya watu wanaojitambua”.







































