Watumishi wa idara ya Fatuma binti Asadi (a.s) chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, wamekamilisha maandalizi ya vikao vya usomaji maalum wa Qur’ani katika mwezi wa Ramadhani.
Maandalizi yamehusisha uandaaji wa sehemu za kufanyia vikao vya usomaji wa Qur’ani, kutoa matangazo, kupanga viti, kuandaa usafiri maalum wa washiriki pamoja na kuandaa misahafu 500.
Idara imeandaa ratiba maalum na kuwagawa wasomaji katika sehemu tatu, ambazo ni: Kituo cha Swidiqatu-Twahirah kutakuwa na usomaji mkuu wa wasichana, Majengo ya makazi ya Abbasi na Muswalla wa Jaamiatul-Amiid, ili kutoa nafasi ya idadi kubwa zaidi ya washiriki.
Idara imetoa mualiko wa jumla kwa kila anaependa kushiriki katika vikao hivyo vya usomaji wa Qur’ani, vitakavyo anza katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.









