Mheshimiwa Sayyid Swafi kawapongeza watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kupokea kipande cha aridhi ya mji wa makazi Alqamaru

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mbeshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amewapongeza watumishi wa Atabatu Abbasiyya kwa kupokea kipamde cha ardhi katika mji wa makazi Alqamaru.

Ametoa pongezi hizo katika upigaji kura ya wazi hatua ya kwanza, ili kuwapata watumishi wa Ataba tukufu watakaopewa viwanja hivyo.

Akasisitiza kuwa Ataba tukufu inafanya kila iwezalo katika kuboresha maisha ya watumishi wake, akasema kuwa watumishi wanastahiki malezi mazuri na kujaliwa.

Akaeleza kuwa Atabatu Abbasiyya imeweka vigezo katika ugawaji wa stahiki mbalimbali kwa watumishi.

Akabainisha kuwa, viwanja hivi vitajengwa nyumba za makazi kama sehemu ya kuonyesha thamani ya mtumishi, kazi ya ujenzi itafanywa na baadhi ya mashirika kutokana na ukubwa wa mji.

Akasema kuwa, anatarajia watumishi wote watakaopata viwanja wanufaike na viwanja vyao kwa kujenga nyumba za kuishi wao na familia zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: