Idara ya Dini tawi la wanawake chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum iitwayo (korido za Ramadhani) kwa zuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kiongozi wa idara Bibi Adhraa Shami amesema: “Idara imeandaa ratiba hiyo kwa lengo la kukuza uhusiano na Ahlulbait (a.s) na kunufaika na mwezi wa Ramadhani kwa kufanya ibada na kukumbushana riwaya zinazohimiza umuhimu wa kuwafuata Ahlulbait (a.s) na kupambana na changamoto za zama hizi”.
Akaongeza kuwa ratiba inahusisha usomaji wa riwaya za Maimamu watakasifu (a.s) na kujadili mafundisho yake pamoja na zuwaru, na namna ya kunufaika na mafundisho ya riwaya hizo katika maisha ya kila siku”.
Washiriki wameonyesha kuridhishwa na ratiba hiyo iliyoandaliwa na idara.







