Kitengo cha utalii wa kidini kimetangaza kurudi kwa msafara wa Saaqi baada ya kukamilisha ibada ya Umra

Kitengo cha utalii wa kidini katika Atabatu Abbasiyya kimetangaza kurudi kwa msafara wa Saaqi baada ya kukamilisha ibada ya Umra.

Msafara huo ulifuatana na mtumishi kutoka idara ya utalii wa kidini na muelekezaji wa mambo ya kidini kutoka kitengo cha Dini wakati wote wa utekelezaji wa ibada hiyo.

Walianza kwa kutoa mihadhara elekezi kuhusu utekelezaji wa ibada ya Umra, namna ya kufanya tawafu, uwekaji wa nia, mambo ambayo ni haram baada ya kufanya ihram, swala ya tawafu na hukumu zingine zinazofungamana na ibada ya Umra pamoja na miongozo ya kiidara.

Kitengo cha utalii wa kidini huratibu misafara mbalimbali ya kidini na kutoa huduma kwa wasafiri ndani na nje ya Iraq, kwa uratibu na ufanisi wa hali ya juu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: