Kitengo cha Dini kimetangaza idadi ya ndoa zilizofungwa katika mwezi wa Shabani

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kimetangaza idadi ya ndoa zilizofungwa katika mwezi mtukufu wa Shabani.

Kiongozi wa mambo ya kijamii chini ya kitengo, Shekhe Muhammad Kuraitwi amesema: Kitengo kimeshuhudia muitikio mkubwa wa kufunga ndoa katika mwezi wa Shabani, akasema kuwa, wamefungisha ndoa zaidi ya 500 katika mwezi huo.

Akaongeza kuwa, kitengo kiliandaa sehemu maalum ya kufungishia ndoa, ikiwa ni pamoja na kutoa mihadhara kuhusu umuhimu wa maisha ya ndoa na mjia za kuwa na utulivu wa kifamilia.

Kitengo cha Dini kinaendelea kutoa huduma za kidini na kujenga misingi imara ya kijamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: