Kitengo kinachosimamia haram kimeanza kutoa huduma maalum za mwezi wa Ramadhani kwa zuwaru

Kitengo kinachosimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya kinatoa huduma maalum kwa zuwaru chini ya ratiba ya mwezi wa Ramadhani.

Makamo rais wa kitengo Sayyid Zainul-Aabidina Adnani Quraishi amesema: “Watumishi wa kitengo wameandaa korido za haram na kuzigawa kwa kuweka vizuwizi ili kuongoza matembezi ya zuwaru, sambamba na kuweka vitabu vya dua maalum za mwezi wa Ramadhani na kubadilisha turba elfu hamsini kwa kuweka zingine mpya”.

Akaongeza kuwa “Huduma zimehusisha uwekaji wa mahitaji ya lazima katika usomaji wa Qur’ani, kama vile kuandaa jukwaa na vitu vingine vinavyohitajika katika swala hilo, bila kusahau upulizaji wa marashi ndani ya haram tukufu”.

Akaendelea kusema “Uwanja wa Bibi Ummul-Banina (a.s) umetandikwa wote kwa kushirikiana na kitengo cha mgahawa ili kurahisisha ugawaji wa futari kila siku”.

Kazi hizo ni sehemu ya mkakati maalum wa kuboresha huduma kwa zuwaru, na kuweka mazingira mazuri kiibada katika mwezi huu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: