Majmaa-Ilmi imefanya mashindano ya Qur’ani awamu ya tisa katika mkoa wa Baabil

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya mashindano ya Qur’ani kwa vikundi awamu ya tisa kupitia program ya kongamano la Multaqa-Nuraini awamu ya tano mkoani Baabil.

Kongamano linasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani katika mkoa wa Baabil chini ya Majmaa, kwa kushirikiana na uongozi maalum wa mazaru ya Alawiyya Sharifa binti Imamu Hassan Almujtaba (a.s).

Mkuu wa Maahadi Sayyid Muntadhiru Mashaikhi amesema: Kamati ya maandalizi ilitangaza kukubali vikosi 12 vinavyohusisha mahafidhu, wasomaji, walimu wa fani za usomaji, tafsiri, miujiza ya Qur’ani na jopo la majaji.

Akabainisha kuwa, upekee wa mashindano ya vikundi ni kusaidiana wanakikundi, kikundi kinakuwa na washiriki wa fani tofauti jambo linalosaidia kujenga utamaduni wa kushirikiana na kutafakari kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: