Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kupitia jumuiya ya Skaut ya Alkafeel, kimetangaza kunufaika kwa wanafunzi 4000 katika program ya (Msimu wa maarifa ya Mahdawiyya ya Skaut) iliyofanywa wakati wa likizo.
Kiongozi mkuu wa jumuiya hiyo Sayyid Ali Asadi amesema “Program ilikuwa na ushiriki mkubwa, zaidi ya watu 4000 wamenufaika na program hiyo.
Akaongeza kuwa, program imesaidia kutumia vizuri kipindi cha likizo, kwa kuweka mazingira mazuri yaliyochukua maelfu ya wanafunzi na familia zao, wametumia muda wao kwa mambo yenye faida za kimalezi na kielimu.
Akafafanua kuwa, Program imejikita katika kuimarisha mahusiano ya kifamilia na kimalezi, aidha program hiyo ni kitovu muhimu cha kuandaa kizazi cha watu wanaojitambua, wenye uwezo wa kuhudumia Dini, Taifa na jamii yao.





