Rais wa kitengo hicho Sayyid Nadhim Alghurabi amesema “Watumishi wa kitengo cha ufundi wamefanya ukarabati wa dirisha la zamani katika malalo ya Maimamu wawili Askariyaini (a.s), kiwango cha ukamilifu kimefika asilimia %90, baada ya kulipeleka kwenye karakana maalum na kukarabati sehemu zilizoharibika baada ya shambulio lililofanywa na magaidi mwaka 2006m”.
Akaongeza kuwa “Hatua za ukarabati zimefanywa kwa utaratibu maalum, wameanza kukarabati sehemu za dirisha zilizotengenezwa mwaka 1962m, kwa kuondoa sehemu zilizo haribika na kuzipeleka katika makumbusho ya Atabatu Askariyya”. Akabainisha kuwa “Ukarabati huo ni sehemu ya makubaliano ya ushirikiano yaliyopo baina ya Ataba mbili tukufu Abbasiyya na Askariyya”.





