Kitengo cha habari na utamaduni kinafanya shindano la kiigizo chema awamu ya tatu

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimetangaza shindano la (kiigizo chema) awamu ya tatu, linalenga kuimarisha utambuzi wa historia tukufu ya Mtume.

Shindano linasimamiwa na Daaru Rasulul-Aadham (s.a.w.w) chini ya kitengo.

Shindano linamaswali 50 kuhusu historia ya Mtume (s.a.w.w), kwa ajili ya kujenga uelewa wa historia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika jamii na kushajihisha usomaji wa historia ili waweze kupambika na maadili yake matakatifu.

Shindano limeanza tarehe 1 Ramadhani 1447h na litaisha tarehe 30 Ramadhani 1447h, washindi kumi wa mwanzo watapewa zawadi katika tukio maalum litakalo pangwa.

Kwa maelezo zaidi piga simu kwa namba zifuatazo: 07602355555
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: