Wahudumu wa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya wanafanya kazi ya kusafisha eneo lote linalozunguka Ataba tukufu na barabara zinazoelekea Ataba ndani ya mwezi huu wa Ramadhani.
Kazi hiyo ni sehemu ya mkakati wa kudumisha usafi na kuweka mazingira mazuri kwa zuwaru ndani ya mwezi wa Ramadhani.
Kazi imehusisha kuondoa uchafu kwenye mapiba ya taka, kusafisha barabara zinazoelekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na vibaraza.
Kitengo cha utumishi kinasimamia usafi katika eneo lote linalozunguka Atabatu Abbasiyya na barabara zinazoelekea Ataba, kwa lengo la kuifanya sehemu hiyo iwe na muonekano mzuri kwa zuwaru.






