Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, kimetoa muhadhara elekezi kuhusu mwezi wa Ramadhani kwa watumishi wa kitengo cha mgahawa (mudhifu) wa Ataba tukufu.
Mhadhiri Shekhe Haidari Aaridhwi amesema: “Muhara unatokana na hutuba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliyotoa wakati wa kukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani”.
Akaongeza kuwa “Muhadhara umeeleza madhumuni ya hutuba ya Mtume (s.a.w.w) na kubainisha matendo mema katika mwezi wa Ramadhani yanamalipo makubwa sana tofauti na mwezi mingine”.
Kitengo cha Dini kinajenga uelewa wa kidini kwa watumishi wa Ataba, kupitia semina mbalimbali na mihadhara elekezi.



