Idara ya masayyid katika Atabatu Abbasiyya, inahudumia zuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika siku za mwezi mtukufu wa Ramadhani kupitia maukibu ya kutoa huduma.
Maukibu ipo katika barabara ya Baadul-Qibla, wanagawa chai na vitafunywa wakati wa usiku katika mwezi mzima wa Ramadhani, kuanzia wakati wa futari hadi daku, jambo hili hufanywa kila mwaka ikiwa ni sehemu ya kuhudumia zuwaru wa malalo takatifu.
Wahudumu wa idara hiyo hutekeleza majukumu ya kiibada ndani na nje ya haram tukufu, ikiwa ni sehemu ya kuhuisha usiku wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, kulingana na mahitaji ya zuwaru na kuwawekea mazingira mazuri.






