Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.. kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili kinagawa sahani elfu 10 za futari kwa zuwaru

Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili katika Atabatu Abbasiyya, kinagawa sahani za futari elfu 10 kwa zuwaru wanaokuja kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala.

Makamo rais wa kitengo Sayyid Habibu Dahashi amesema “Watumishi wa kitengo wanagawa sawani za futari elfu 10 kwa zuwaru, katika maeneo tofauti ndani ya mji wa Karbala.

Akaongeza kuwa “Sehemu za ugawaji wa futari ni (Mlango wa Baghdad, barabara ya Alqami na barabara ya Abbasi) pamoja na sehemu zinazozunguka Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa lengo la kufikia idadi kubwa zaidi ya zuwaru".

Akasema kuwa “Kitengo kimeandaa vituo vya kugawa maji ya kunywa katika maeneo hayo, kwa lengo la kutoa huduma bora kwa zuwaru, na kuweka mazingira yanayoendana na mwezi huu mtukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: