Watumishi wa kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya Ataba mbili tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kimeandaa eneo la katikati ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kuwa sehemu maalum ya kuhudumia zuwaru.
Makamo rais wa kitengo hicho, Sayyid Ausi Twahiri Mahadi amesema: Watumishi wa kitengo wanaendelea kuhudumia zuwaru wa malalo mbili takatifu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Akaongeza kuwa “Miongoni mwa kazi zinazofanywa kila siku na kitengo hiki ni kutandika zaidi ya zulia 1500 katika eneo la katikati ya haram mbili, pamoja na kutandika mbele ya milango inayoelekea sehemu hiyo, mlango wa Qibla, mlango wa Baghdad na mlango wa Alqami”.
Kazi hiyo ni sehemu ya mkakati wa kutoa huduma bora kwa zuwaru, inayoendana na ukubwa wa idadi ya watu wanaokuja katika mwezi huu mtukufu.







