Atabatu Abbasiyya imeandaa warsha ya hati ya kiarabu na kiislamu katika shughuli za maonyesho ya Qur’ani kimataifa awamu ya tatu jijini Tehran.
Mwanahati wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Karaar Mussawi amesema “Hakika warsha ya hati za kiarabu na kiislamu iliyoandaliwa na Ataba tukufu katika tawi lake, ni sehemu ya maonyesho ya kimataifa jijini Tehran, imetembelewa na wanahati wakubwa wa Iran, akiwemo Sayyid Muhammad Ridha Dhwarifu.
Akaongeza kuwa, Warsha imehusisha uandishi wa aya za Qur’ani tukufu na hadithi za Ahlulbait (a.s) mbele ya zuwaru.
Tawi la Atabatu Abbasiyya limeonyesha machapisho ya kielimu kutoka Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu sambamba kuweka shughuli za kivitengo kwa zuwaru wa tawi.





