Kitengo cha mgahawa kinatoa sahani elfu 6 za futari kwa zuwaru wa mji mtukufu wa Karbala

Kitengo cha mgahawa katika Atabatu Abbasiyya kinatoa sahani elfu 6 za futari kwa zuwaru wa mji wa Karbala kupitia mkakati wake maalum wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kitengo kimeandaa utaratibu wa kugawa futari kwa zuwaru siku zote za mwezi huu mtukufu, pamoja na kuweka mpango-kazi unaowezesha kutoa huduma bora.

Watumishi wa kitengo katika usiku wa Ijumaa ya pili ya mwezi wa Ramadhani wamegawa sahani za futari elfu 6 kwa zuwaru, katika mazingira ya kuongezeka idadi ya watu wanaokuja kufanya ziara katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mkakati unahusisha ugawaji wa futari na daku kwa watumishi wa Ataba, kama sehemu ya kuunga mkono juhudi zao za kuhudumia zuwaru na kuhuisha mazingira ya mwezi huu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: