Jumuiya ya kielimu Al-Ameed inatoa mihadhara ya kidini na usomaji wa Qur’ani katika mwezi wa Ramadhani.
Ratiba hiyo inafanywa kwa kushirikiana na kituo cha kimataifa Al-Ameed chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Muhadhara umetolewa na rais wa jumuiya Dokta Sarhani Jafaati Salmaan, ameongea kuhusu umuhimu wa kufunga na utukufu wa mwezi wa Ramadhani, akaangazia mambo ya kiroho na kijamii, na nafasi ya funga katika kutakasa nafsi na kukuza Imani kwa mtu na jamii.
Ratiba inamihadhara yenye mada tofauti kuhusu mwezi mtukufu wa Ramadhani na mwenendo halisi wa waislami katika mazingira ya kila siku.
Vikao vya usomaji wa Qur’ani vinaendelea katika ofisi za jumuiya, siku zoto za mwezi mtukufu wa Ramadhani.




