Kupitia madirisha tofauti.. kitengo cha mgahawa kinagawa futari kwa zuwaru wa mji wa Karbala

Kitengo cha mgahawa katika Atabatu Abbasiyya kinagawa futari kwa zuwaru wa mji wa Karbala kupitia madirisha mbalimbali.

Wahudumu wa kitengo cha mgahawa wanagawa maelfu ya sahani za futari kila siku kwa zuwaru wa malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Wanagawa futari na daku kupitia madirisha yaliyoandaliwa kabla, jambo linalosaidia mtiririko mzuri na ubora wa huduma kwa zuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: