Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili kimeweka mabango yanayoashiria huzuni katika kumbukizi ya kifo cha Bibi Khadija (a.s)

Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili katika Atabatu Abbasiyya, kimeweka mabango yanayoashiria huzuni kufuatia kumbukizi ya kifo cha Bibi Khadija (a.s).

Watumishi wa kitengo wameweka mabango yaliyoandikwa maneno ya kuomboleza kifo cha Bibi Khadija (a.s), kama sehemu ya kumpa pole Mtume Muhammad (s.a.w.w), na kuenzi msimamo wake katika kunusuru Dini ya kiislamu, mabango hayo yamewekwa katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu.

Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya program ya kitamaduni na maombolezo, sambamba na kujenga uwezo wa uelewa wa misingi ya uislamu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: