Sayyid Sistani ametuma salam za rambirambi kufuatia kuuawa kishahidi kwa Sayyid Khamanei

Marjaa-Dini mkuu Muheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani, ametuma salam za rambirambi kwa raia wa Iran na waislamu wote kwa ujumla kufuatia kuuawa kishahidi kwa Ayatullah Sayyid Ali Khamanei.

Nakala ya tomko inasema:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

(Hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea)

Kwa majonzi makubwa tunawapa pole raia wa Iran na waislamu wote kwa kuuawa kishahidi kiongozi mkuu wa jamhuri ya kiislamu ya Iran Muheshimiwa Ayatullah Sayyid Khamanei (r.a).

Hakika nafasi kubwa ya Muheshimiwa katika uongozi wa jamhuri ya kiislamu ya Iran na upekee wake katika taifa hilo kwa miaka mingi upo wazi, bila shaka maadui wamelenga kumuua na kuanzisha vita kubwa katika taifa la Iran ili walidhuru taifa hilo tukufu, tunatarajia raia watukufu wa Iran walinde umoja wao na kupanga safu zao, wala wasiruhusu maadui kufikia lengo lao ovu.

Namuomba Mwenyezi Mungu amuweke mahala pema peponi na awape subira na utulivu raia wa Iran na waislamu wote kwa ujumla.

Hakuna hila wala nguvu ispokua zinatoka kwa Mwenyezi Mungu mkuu.

(11. Ramadhani/ 1447h) sawa na tarehe (1 Machi/ 2026m).

Ali Husseini Sistani
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: