Kitengo cha uboreshaji kimekamilisha semina ya habari kwa watumishi wake

Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya, kimekamilisha semina ya habari kwa watumishi wake.

Mkufunzi wa semina alikuwa ni Sayyid Ali Hasuun Shimri, ameongea mada mbalimbali, miongoni mwake ni: Misingi ya kuonekana mbele ya kamera, lugha ya muili, uendashaji wa mazungumzo kihabari, uandaaji wa jumbe kuu na mbinu za kuamiliana na maswali ya moja kwa moja.

Semina imedumu kwa muda wa siku nne, saa tatu za masomo kila siku, imehitimishwa kwa kufanya mtihani wa nadhariya na vitendo ili kupima uelewa wa washiriki.

Semina hii ni sehemu ya mkakati wa kujenga uwezo wa watumishi katika sekta ya habari na kuimarisha utendaji wa kitaasisi katika jukwaa tofauti za habari chini ya malengo ya kitaasisi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: