Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa program ya kitamaduni kwa wageni kutoka kitivo cha malezi na elimu katika chuo kikuu cha Karbala.
Sayyid Alawi Hussein amesema, “Miongoni mwa harakati zetu ni kukaribisha wageni kutoka ndani na nje ya Iraq, tumepokea wageni kutoka kitivo cha malezi na elimu katika chuo kikuu cha Karbala, ukiwa na watu 50”.
Akaongeza kuwa “Idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule imeandaa ratiba inayohusisha ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s), matembezi katika makumbusho ya Alkafeel, kisha kuangalia miradi ya Ataba tukufu”.
Akafafanua kuwa “Ratiba imehusisha kutembelea mradi wa ukanda wa kijani kibichi, wageni wamesikiliza maelezo kutoka kwa rais wa kitengo Mhandisi Nasoro Hussein Mut’ibu kuhusu sehemu za kilimo na utendaji kazi wake, mradi wa kilimo unakusanya baina ya utunzaji wa mazingira na kuweka muonekano mzuri wa kitalii”.





