Miongoni mwa program za kuhuisha mwezi mtukufu.. idara ya wahadhiri wa Husseiniyya imeandaa majlisi na kutoa mawaidha na maelekezo

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya, imefanya majlisi na kutoa mawaidha na maelekezo, kupitia program maalum ya tablighi katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Majlisi imefanywa baada ya futari, imehudhuriwa na kundi kubwa la waumini wanaokuja kuhuisha mwezi huu mtukufu na kunufaika na madhumuni ya kiimani.

Mhadhiri alikuwa ni Shekhe Fadhili Haidari, ameongea kuhusu utukufu wa mwezi wa Ramadhani na ametoa maelekezo mbalimbali yanayo imarisha misingi ya kidini na mahusiano ya Qur’ani na mwenendo wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: