Wahudumu wa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya, wamefanya usafi kwenye barabara zinazozunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kazi hiyo ni sehemu ya mkakati wa kudumisha usafi na kuweka mazingira mazuri wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kitengo cha utumishi kinadumisha usafi katika eneo lote linalozunguka Atabatu Abbasiyya na barabara zinazoelekea eneo hilo, ili kuweka muonekano mzuri unaoendana na utukufu wa sehemu na zuwaru wake.



