Wasomaji 30 wameshiriki katika kusoma Qur’ani khitima 18 ndani ya mwezi wa ramadhani katika mkoa wa Diwaniyya

Wasomaji thelathini wanasoma khitima kumi na nane ndani ya mwezi wa Ramadhani, katika misikiti tofauti ndani ya mkoa wa Diwaniyya.

Vikao vya usomaji wa Qur’ani ndani ya mwezi wa Ramadhani vimeratibiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa-Ilmi katika Atabatu Abbasiyya.

Usomaji wa Qur’ani unafanywa kwenye misikiti mbalimbali ndani ya mkoa na wilaya ya Shamia, Sumar na mtaa wa Nafar.

Usomaji wa Qur’ani ni sehemu ya mkakati wa Majmaa-Ilmi, unaolenga kusambaza utamaduni wa kusoma Qur’ani katika maeneo tofauti ya mkoa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: