Ukumbi wa haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika usiku wa Ijumaa ya kwanza ndani ya mwezi wa Shawwal, umeshuhudia usomaji wa dua Komail kwa ushiriki wa kundi kubwa la zuwaru.
Usomaji wa dua umefanywa katika mazingira tulivu ya kiimani, kwa ushiriki wa zuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wameweka mazingira mazuri ya utekelezaji wa ibada hiyo kila wiki, wameandaa vitabu vya dua, sehemu maalum ya kufanyia idaba, wamepuliza marashi pamoja na kutoa huduma mbalimbali.







