Kitengo cha maelekezo ya kinafsi na kimalezi (saikolojia) katika chuo kikuu cha Alkafeel, kimefanya majlisi ya kuomboleza kumbukizi ya kuvunjwa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s).
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Ali Zubaidi kutoka Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa-Ilmi katika Ataba tukufu, ukafuata muhadhara wa kidini kutoka kwa Mheshimiwa Sayyid Jafari Muruji, ameongea kuhusu hadhi ya malalo takatifu na umuhimu wa kuzitunza kwani ni sehemu muhimu ya utambulisho wa Uislamu.
Akasisitiza umuhimu wa kupambana na fikra potofu zinazolenga kubomoa maeneo matakatifu, akahimiza kujenga uelewa, misingi ya kidini na kibinaadamu katika jamii.
Chuo kikuu cha Alkafeel huadhimisha matukio mbalimbali ya kidini, kwa kufanya program zinazolenga kuimarisha uelewa wa mafundisho ya Dini na utamaduni kwa wanafunzi na jamii.




