Kituo cha afya na Amani Alkafeel chini ya kitengo cha tiba katika Atabatu Abbasiyya kimefanya warsha ya utoaji wa huduma za uokozi kwa watumishi wa Ataba tukufu.
Mkufunzi bwana Ahmadi Nadhim amesema: “Kituo kimeanza kufanya warsha za kuwafundisha watumishi utoaji wa huduma za uokozi” akabainisha kuwa “Warsha imefanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Mahadi (a.f) kwa muda wa siku mbili”.
Akaongeza kuwa “Warsha imehusisha mafunzo ya uokozi kwa watu wenye tatizo la moyo, namna ya kumsaidia mtu aliyezimia, mkubwa, kijana na mtoto”.
Akabainisha kuwa “Lengo la semina hii ni kujenga uwezo wa watumishi katika sekta ya uokozi, ili waweze kutoa huduma bora ya afya kwa zuwaru”.







