Idara ya Dini tawi la wanawake imefanya program ya kila wiki Miftahul-Baswirah

Idara ya Dini tawi la wanawake chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, imefanya program ya kila wiki (Miftahul-Baswirah).

Kiongozi wa idara hiyo bibi Adhraa Shami amesema: “Program imelenga kubainisha hukumu za kifiqhi kwa watumishi wa kike katika Ataba tukufu, chini ya utaratibu wa kukuza uelewa wa Dini”.

Akaongeza kuwa “Program inahusisha maelezo ya kina kuhusu hukumu za kifiqhi kwa wanawake, ili kuwafanya waelewe kwa usahihi hukumu za kisheria”.

Program hiyo ni sehemu ya harakati za kielimu zinazofanywa na idara, kwa lengo la kuimarisha elimu ya Dini kwa watumishi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: