Jumuiya ya mwezi mwekundu nchini Iran imesema: Tunathamini sana msimamo ya Marjaa-Dini mkuu na raia wa Iraq katika siku hizi ngumu

Jumuiya ya mwezi mwekundu nchini Iran imeshukuru msimamo wa Marjaa-Dini mkuu katika mji wa Najafu, raia wa Iraq na Ataba tukufu kutokana na hali ngumu inayopitia kwa sasa jamhuri ya kiislamu ya Iran.

Kiongozi mkuu mtendaji wa jumuiya ya mwezi mwekundu nchini Iran, Sayyid Muhammad Kabadi amesema: “Taasisi ya misaada na uokozi chini ya jumuiya jenye makao makuu jijini Tehran, inathamini sana msaada wa kimaanawiyya unaotolewa na Marjaiyya, akiwemo Marjaa-Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani na raia wengine woto wa Iraq tukufu, hali kadhalika jitihada kubwa inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika siku hizi ngumu”.

Akaongeza kuwa “Msimamo wa kushikamana na raia wa Iran unaofanywa na watu wa Iraq ni jambo kubwa sana”.

Atabatu Abbasiyya imetuma msafara wa misaada ya kibinaadamu kwa ajili ya kusaidia watu wa Iran na Lebanon, ikiwa ni sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa-Dini mkuu, msafara ulikuwa na tani 690 za misaada mbalimbali ya kibinaadamu, tani 670 za bidhaa za chakula na tani 20 za vifaa-tiba.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: