Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili kinatoa huduma ya kubeba zuwaru wazee na wenye ulemavu kupitia gari za kuchaji

Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili katika Atabatu Abbasiyya, kinatoa huduma ya kubeba zuwaru wazee na watu wenye ulemavu kupitia gari za kuchaji.

Rais wa kitengo Sayyid Hussam Hussein amesema: Huduma hiyo ni sehemu ya kurahisisha ufikaji wa zuwaru katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kufanya ibada tukufu ya ziara.

Akaongeza kuwa, huduma ya gari za kuchaji inatolewa kwenye malango matano yanayoingia katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na mlango wa barabara ya Jamhuriyya.

Kazi hiyo hufanywa chini ya utaratibu maalum ulioandaliwa na kitengo, kwa ajili ya kutoa huduma bora zaidi kwa zuwaru na kuandaa mazingira mazuri ya kufanya ziara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: