Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya majlisi ya kuomboleza misiba ya Ahlulbait (a.s) ndani ya ukumbi wa utawala.
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ukafuata muhadhara wa kidini kuhusu misiba waliyopata Ahlulbait (a.s) na umuhimu wa kushikamana nao na kufuata mwenendo wao mtukufu.
Kitengo hufanya majlisi za kuomboleza kwa lengo la kuhuisha kumbukizi ya Ahlulbait (a.s) na kusambaza elimu na utukufu wao sambamba na kusisitiza kufuata mwenendo wao mtukufu.









