Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimechapisha kitabu kipya chenye anuani isemayo (Maisha ya kiislamu na nyenzo za maarifa), kilichoandikwa na Dokta Muhammad Kawiyani.
Kitabu hicho ni sehemu ya mfululizo wa masomo ya maisha, yanayotolewa na idara ya tafiti za kiislamu na kimkakati chini ya kitengo, aidha ni sehemu ya mkakati wa kuongeza vitabu vya kielimu katika maktaba.
Kitabu kimeandika mambo yanayohusiana na maisha bora katika mtazamo wa kiislamu, muandishi ameangazia mambo mbalimbali ya kielimu, ameandika kuhusu misingi ya nadharia ya maisha bora kwa undani.
Kitabu kimesheheni tafiti za kielimu katika kufafanua misingi ya maisha bora katika uislamu, kinajenga uelewa zaidi kwa msomaji.
