Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili kimeweka mabango yanayoashiria huzuni kufuatia kumbukizi ya kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s)

Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili katika Atabatu Abbasiyya, kimeweka mabango yanayoashiria huzuni kufuatia kumbukizi ya kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s).

Eneo la katikati ya haram mbili tukufu limewekwa mabango meusi yanayoashiria msiba na kumbukizi ya historia ya Imamu Swadiq (a.s) na dhulma alizofanyiwa.

Uwekaji wa mabango hayo ni sehemu ya maandalizi ya Atabatu Abbasiyya ya kuomboleza msiba huo mkubwa, na kupokea zuwaru wanaokuja kushiriki kwenye maombolezo hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: