Kitengo cha mahusiano kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Swadiq (a.s)

Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya majlisi ya kuomboleza kumbukizi ya kifo cha Imamu Jafari Swasiq (a.s).

Majlisi imefanywa katika ukumbi wa utawala ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhuduriwa na idadi kubwa ya watumishi wa Ataba na zuwaru.

Mtoa muhadhara na kiongozi wa idara ya wahadhiri katika Atabatu Abbasiyya Shekhe Abdu Swahibu Twaiy amesema, “Siku hizi zinashuhudia majlisi ndani ya Ataba tukufu, kuomboleza kumbukizi ya kifo cha Imamu Swadiq (a.s) kutokana na utukufu wake katika umma wa kiislamu”.

Akaongeza kuwa “Majlisi imeangazia historia ya Imamu Swadiq (a.s) na nafasi yake katika kufundisha Dini, hakika alikuwa kitovu cha elimu na hekima”.

Akabainisha kuwa “Majlisi inalenga kuimarisha uwelewa wa kidini na kuomboleza msiba huo mkubwa katika nafsi za waumini”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: