Maukibu imeshuhudia ushiriki wa wajumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya, viongozi wa vitengo na watumishi.
Maukibu imefanya matembezi ya Amani kuanzia ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakapita uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, wakaenda hadi ndani ya malalo ya Imamu Hussein (a.s) kuomboleza msiba huo, waombolezaji wameimba qaswida na tenzi za uombolezaji zilizoamsha hisia ya huzuni na majonzi.
Wahudumu wa Ataba mbili tukufu huadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s), kama vile tarehe za kuzaliwa na kufa kwao ndani ya kipindi cha mwaka mzima kwa kufanya maukibu ya pamoja.












