Kitengo cha mgahawa kimetoa huduma kwa zuwaru katika kumbukizi ya kifo cha Imamu Swadiq (a.s)

Kitengo cha mgahawa katika Atabatu Abbasiyya, kimehudumia zuwaru wa malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kumbukizi ya kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s).

Miongoni mwa huduma zilizotolewa na kitengo hicho kwa zuwaru ni, ugawaji wa chakula, vinywaji baridi na zinginezo, ikiwa ni katika mkakati maalum wa kuomboleza msiba huo.

Ugawaji wa chakula umefanywa katika utaratibu bora, yanayojali afya na mpangilio.

Atabatu Abbasiyya imeandaa mazingira mazuri kwa zuwaru kwa kuzingatia mahitaji yao, hufanya hivyo kwenye matukio yote ya kidini yanayoadhimishwa hapa Karbala, likiwemo tukio hili la kumbukizi ya kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: