Idara ya Bibi Fatuma binti Asadi (a.s) ya masomo ya Qur’ani, chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, imeomboleza kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s) kupitia majlisi ya kuomboleza.
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ukafuata muhadhara kuhusu historia ya Imamu Swadiq (a.s) na nafasi yake katika sekta ya elimu kwa kuanzisha madrasa ya Jaafariyya ambayo matunda yake yameenea sehemu mbalimbali ya dunia, pamoja na vikwazo vya zama hizo.
Idara hufanya program zinazochangia kujenga misingi ya kiislamu na kufundisha mwenendo wa Ahlulbait (a.s), kwa namna ambayo inaimarisha uelewa wa Dini na kukuza nafasi ya mwanamke katika kuhamisha ujumbe kizazi hadi kizazi.





